Friday, April 17, 2015


Mechi za Jumamosi za Nusu Fainali ya FA CUP na Bigi Mechi ya Ligi Kuu England ambazo zote zitachezwa Jijini London huko Uingereza zimezua tafrani kubwa baada ya kutokea mgonganoo kwa sababu tu ya matakwa ya Makampuni ya TV.
Jumamosi Uwanjani Wembley itachezwa Nusu Fainali ya Kombe kubwa na kongwe ya FA CUP kati ya Reading na Arsenal kuanzia Saa 1 na Dakika 20 Usiku kwa Saa za Bongo na Dakika 10 baadae huko Stamford Bridge itaanza Bigi Mechi ya Ligi Kuu England kati ya Chelsea na Manchester United.

Huko Uingereza, Mechi ya Nussu Fainali ya FA CUP ya Reading v Arsenal itaonyeshwa na TV ya BBC1 na ile ya Ligi ya Chelsea v Man United itarushwa na Sky Sports.Kutokutenganishwa kwa muda wa kuanza Mechi hizi kumezua mjadala mkubwa huko England na Wadau mbalimbali kuponda uroho wa Makampuni ya TV katika ushindani wao.
Akiongelea kuhusu mgongano huo, Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal, ameponda uamuzi wa kuzigonganisha Nusu Fainali ya FA CUP na Mechi kubwa ya Ligi.
Amesema: "Lazima wangefanya uamuzi. Hili halipaswi kutokea katika Nchi moja. Kombe kubwa la FA CUP linagonganishwa na Mechi kubwa ya Ligi!"
Jack W. kwenye mazoezi
Kocha Arsene Wengerakiwacheki Vijana wake kwenye Mazoezi wakijiandaa dhidi ya Timu ya Reading kesho jumamosi usiku saa 1 na dakika 20.Mesut OzilHector BellerinAlexis Sanchez of Arsenal during a training session at London Colney Alexies SanchezWojciech Szczesny of Arsenal during a training session at London Colney
Kipa wa Arsenal Wojciech Szszesny

Laurent na Santi Cazorla
Jack Whilshere
Sant Cazorla

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog