Klabu ya Manchester United imeanzisha mazungumzo na ajenti wa Christiano Ronaldo kwa lengo la kumrudisha Old Trafford.
Siku za usoni za Ronaldo zimejaa uvumi huku kukiwa na madai kwamba mchezaji huyo hafurahii maisha ya Madrid.
Habari hizo zimeifungua macho United na sasa ripoti nchini Uhispania zinasema kuwa Manchester United imeanzisha mazungumzo na ajenti wa mchezaji huyo Jorge Mendes kwa lengo la kumrudisha mchezaji huyo Old Trafford.Kulingana na gazeti la Metro nchini Uingereza United ina matumaini ya kumpata Ronaldo kwa kitita cha yuro millioni 100 ambazo ni sawa na pauni millioni 71.1.
0 maoni:
Post a Comment