Sunday, March 15, 2015



Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa mashindano ya NSSF Media Cup 2015, yaliyoanza kulindima katika viwanja vya Sigara, Chang'ombe Dar es Salaam leo asubuhi.

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akihutubia baada ya kufungua mashindano hayo.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (katikati), akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali waliohudhuria ufunguzi wa mashindano hayo. Kutoka kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,Ludovick Mrosso, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini NSSF, Abubakar Rajab, Mkurugenzi Rasilimali Watu, Chiku Matessa na Mkurugenzi wa Uthamini na Usimamizi wa Hadhara, Sadi Shemliwa.

Kikosi cha Timu ya Free Media kilichofungua mashindano hayo kwa kucheza na Shirika la Utangazaji Tanzania TBC.

Kikosi cha Shirika la Utangazaji Tanzania TBC kilichomenyana na Free Media na kuibuka washindi wa bao 1-0 na kuendelea na mashindano hayo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog