Friday, August 15, 2014


MENEJA wa Crystal Palace Tony Pulis ameondoka Crystal Palace ikiwa ni Siku mbili tu kabla Msimu mpya wa Ligi Kuu England kuanza.
Pulis, mwenye Miaka 56, amebwaga manyanga baada ya kukorofishana na Mwenyekiti Steve Parish kuhusu ununuzi wa Wachezaji wapya kwa ajili ya Msimu mpya.
Pulis alikuwa Meneja wa Stoke City na kuondoka Klabu hiyo baada ya Miaka 7 ambayo alimudu kuibakisha Ligi Kuu England.

Novemba 2013, Pulis alipewa Umeneja Crystal Palace baada ya kuondoka Ian Holloway na kuiacha Timu iko mkiani lakini Pulis aliibeba Timu na kuanza tena kushinda kwa kuipiga Chelsea 1-0 na kushinda Mechi zao 5 mfululizo zilizofuata.
Moja ya Mechi zao maarufu Msimu uliopita ni ile dhidi ya Liverpool ambayo walikuwa wameshafungwa Bao 3-0 zikiwa zimebaki Dakika 11 lakini wakasawazisha Bao zote na huo ukawa mwanzo wa mwisho wa Liverpool kuota Ubingwa.
Matokeo hayo yalimfanya Pulis aisaidie Crystal Palace kumaliza Nafasi ya 11 kwenye Ligi Kuu England kitu ambacho walikuwa hawajawahi kufikisha tangu 1992.
Award winner: Tony Pulis was named Barclays Premier League manager of the season
Palace imesema aliekuwa Meneja Msaidizi Keith Millen ndie ataongoza Timu wakati Jumamosi itaenda huko Emirates kucheza na Arsenal katika Mechi ya kwanza ya Msimu mpya wa Ligi Kuu England.


Kocha huyo  Pulis amechukizwa na ametatizwa kwenye jambo zima la kuhusu Ununuzi wa Wachezaji wapya katika klabu hiyo ya Crystal Palace

Aliyekuwa kocha wa Crystal Palace ambapo kwa sasa amemwaga manyanga!

Kipindi cha Nyuma Meneja huyo Tony Pulis akimpa maelekezo ya hapa na pale Marouane Chamakh kwenye mchezo wa kirafiki kati yao na  Augsburg

Steven Caulker alitakiwa na Palace lakini alijiunga na wazee wa London QPR ambao pia na mahasimu wao!


RATIBA MECHI ZA UFUNGUZI - LIGI KUU ENGLAND
Jumamosi Agosti 16
14:45 Man United v Swansea [Old Trafford]
17:00 Leicester v Everton [King Power Stadium]
17:00 QPR v Hull [Loftus Road Stadium]
17:00 Stoke v Aston Villa [Britannia Stadium]
17:00 West Brom v Sunderland [The Hawthorns]
17:00 West Ham v Spurs [Boleyn Ground]
19:30 Arsenal v Crystal Palace [Emirates Stadium]

Jumapili Agosti 17
15:30 Liverpool v Southampton [Anfield]
18:00 Newcastle v Man City [St. James' Park]

Jumatatu Agosti 18
22:00 Burnley v Chelsea [Turf Moor]

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog