Friday, August 15, 2014

index

KLABU 12 za timu za soka za maveterani zinazooundwa na nyota wa zamani wa kandanda nchini zinatarajiwa kuchuana katika michezo maalum ya Tamasha la Miaka 16 ya Home Gym, itakayofanyika Septemba 6 kwenye uwanja wa Mwenge, Dar es Salaam.
Aidha zaidi ya klabu 30 za Jogging nazo zinatarajiwa kupamba tamasha hilo ambalo litahusisha pia michezo mbalimbali ikiwamo ya netiboli, kuvuta kamba, kukimbia kwenye magunia na kukimbiza kuku.
Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo, Andrew Mangomango, klabu za maveterani zilizothibitisha kushiriki tamasha hilo ambalo litapambwa na burudani ya muziki na shoo ya watunisha misuli, wanyanyua vitu vizito, ngumi na karateka ni Mbagala Veterani, Boko, 501, Break Point, Survey, Mwenge na Msasani.
Mangomango alizitaja nyingine kuwa ni Biafra Veterani, Meeda, Mikocheni, Mbezi, Mabenzi, Segerea na Ukonga Veterani ambazo zinaundwa na nyota wa zamani wa kandanda waliowahi kutamba na timu kama za Simba, Yanga na Taifa Stars.
Juu ya klabu za Jogging mratibu huyo alizitaja kuwa ni pamoja na Temeke Jogging, Mwananyamala, Kingungi, Amani, Magenge, Makuka, 501, Ndiyo Sisi, Wastaarab, Makutanom, Pasada, FBI, Kongowe, Oysterbay Police, Zakheem, Kwa Nyoka, Kawe Beach, Satojio, Kawe Mkwamani na nyingine.
Mangomango aliongeza kuwa baada ya michezo yote wanamichezo washiriki watajumuika pamoja kuwatembelea yatima wanaolelewa kituo cha Chakuhama kwa ajili ya kuwapeleka misaada mbalimbali.
“Ni tamasha ambalo litaambatana na michezo mbalimbali kama ya kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kukimbia kwenye magunia, na shoo za watunisha misuli, wanamieleka, mabondia na karateka kisha kwenda kutembelea yatima,” alisema.
Mangomango alisema mgeni rasmi wa shughuli zote hizo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi cha 501, J.B Kapumbe.
Hii ni mara ya pili kwa tamasha hilo kufanyika mwaja jana lilifanyika wakati Home Gym ikiadhimisha miaka 15 tangu kuasisiwa kwake ambapo shughuli zake kuu ni kufanyisha mazoezi na kutoa ushauri juu ya afya ya mwili.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog