Daniel Sturridge akiwa na tuzo ya Mchezaji Bora wa Februari
MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Daniel
Sturridge ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya England kwa
mwezi Februari, baada ya kufunga mabao matano katika mechi nne.Nyota huyo ameisaidia Liverpool kushinda dhidi ya Swansea na Fulham pamoja na kuitandika mabao 5-1 Arsenal timu hiyo ya Anfield ikiweka hai matumaini ya kutwaa ubingwa.
Sam Allardyce ameiongoza West Ham kuingia kwenye 10 Bora kwa kushinda mechi nne mwezi uliopita
Kocha wa West Ham, Sam Allardyce, ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi baada ya kuiongoza timu yake kushinda mechi nne.
0 maoni:
Post a Comment