Nicolas
Anelka ametamka kuwa hawezi kuomba msamaha kwa klabu yake ya West Brom
juu ya tuhuma za kibaguzi anazoshutumiwa. Tuhuma alizopewa Anelka na
klabu yake ni kuhusiana na aina ya ushangiliaji ambao klabu yake imesema
unakashifu na kubagua jamii fulani ya watu. Kutokana na kufanya kitendo
hicho, cha ushangiliaji kwa kuweka mkono kifuani kama ambavyo
anaonekana kwenye picha, klabu yake imempa adhabu ya kukaa benchi mechi
tano jambo ambalo Anelka mwenyewe amelikataa na amesema atavunja mkataba
wake na West Brom kama watamlazimisha kuomba msamaha na kutumikia
adhabu.
0 maoni:
Post a Comment