Tuesday, February 11, 2014



WAKATI  wafanyabiashara  wakiapa  kuendelea na mgomo wao hadi siku ya jumatano baada ya  kukutana na mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa na mkuu wa mkoa wa Iringa pamoja na TRA ,jeshi la polisi  mkoani hapa  limewataka  wafanyabiashara  wanaotaka kufungua maduka yao kufungua  bila kutishwa na mtu na kama  wanataka  kufikisha  taarifa  polisi  ili  kupewa  ulinzi wa  jeshi  hilo.
Kamanda  wa polisi  mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi ametoa kauli  hiyo wakati akizungumza na mtandao  huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuhusiana  kuwepo kwa  vitisho vya kikundi  cha vijana wanaojiita watoto wa mbwa mwitu  ambao  wanaongoza  wa wafanyabiashara  mjini hapa.
Kamanda  Mungi  alisema  kuwa ni  ruksa kwa mfanyabiashara  yeyote  kufungua  biashara  yake kwa uhuru  na kama kuna  mtu atapita kumtisha anapaswa  kupiga  simu  polisi ili  kuchukua hatua kwa  watoa  vitisho hao .
Kwani alisema ni uhuru  wa mfanyabiashara  kufungua biashara  yake ama kutofungua na kuwa  mtu mwingine  asitumie  nguvu  kumlazizisha mwingine  kufunga ama kufungua.
Kamanda Mungi  alitangaza namba yake ya  simu kwa ajili ya  wafanyabiashara  kutoa taarifa  pale  wanapotishwa kuwa ni 0754612948
Wakati  jeshi la  polisi  mkoa wa Iringa  likitoa taarifa  hiyo ya kuwataka  wafanyabiashara  kuwa huru  kufungua maduka  yao  baadhi ya  wafanyabiashara  eneo la Ipogolo, Mlandege, Kihesa na katikati ya mitaa ya mji  wa Iringa  walionyesha  kususia mgomo  huo na kuendelea na biashara kama kawaida.
Mbali ya  wafanyabiashara  hao kugomea  mgomo  huo kwa madai  kuwa kila mmoja anajua marejesho  yake  benk ya maeneo  mengine  bado  maeneo ya uhindini na Miyomboni kwa mara ya kwanza usiku  wa  leo wafanyabiashara  walioshindwa  kufanya biashara  mchana  walionekana kufungua maduka  yao  hadi saa 4 usiku  tofauti na siku nyingine ambapo maduka hufungwa  saa 12 hadi saa moja  usiku.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog