Saturday, January 18, 2014




LIVERPOOL leo wametoka nyuma ya bao 2-0 Aston Villa bao zimefungwa na Andreas Weimann ambaye amefunga bao la kwanza katika dakika ya 25 na bao la pili likifungwa na Christian Benteke bao safi la kichwa baada ya mlinda mlango wa Liverpool kuukosa na mchezaji mwingine na hatimae Christian Benteke kumalizia bao hilo nyavuni katika dakika 36.
Dakika ya 53 kipindi cha pili liverpool wamepata bahati baada ya Suarez kujiangusha kwenye box na hatimaye Mwamuzi J. Moss kudai ni penati na mkwaju huo wa penati umefungwa na kapteni wa Liverpool Steven Gerrard. Sare hii inawabakisha hapo hapo katika nafasi ya nne Liverpool wakisubiri mtanange wa kesho kutwa jumatatu wa West Brom na Everton matokeo yake. Kama Everton watashinda watawaondoa katika nafasi hiyo ya nne.
 
 
Mmiliki wa Klab ya Liverpool John Henry
 
 

 


 
 
MATOKEO YA  JUMAMOSI:
Jumamosi Januari 18

Sunderland 2 v Southampton 2
Arsenal 2 v Fulham 0
Crystal Palace 1 v  Stoke 0
Man City 4 v Cardiff 2
Norwich 1 v Hull City 0
West Ham 1 v Newcastle 3
Liverpool 2 v Aston Villa 2

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog