Saturday, September 21, 2013

BAADA ya Chelsea kucheza mechi nne katika mashindano yote bila kupata ushindi, Jose Mourinho ameibuka na kusema chanzo cha yote hayo ni mmiliki wa timu hiyo, Roman Abramovich. Mourinho amesema shauku ya bilionea huyo kutaka kuona timu inatandaza soka ya kuvutia dimbani ndiyo chanzo cha matatizo yote. 
“Hatufungi mabao, hiyo ni dhahiri,” alisema Mourinho. 

“Huwezi kusema hatufungi mabao kwa sababu siyo timu ya kushambulia na haichezi soka ya kushambulia, na hatumiliki mpira, kwa sababu tuna mawazo ya kushambulia. 

“Nahisi tunakwenda katika mwelekeo mmoja, ni mwelekeo ambao tunataka kuwa tunacheza aina fulani ya mpira (kutandaza pasi kama Barcelona), lakini ukweli ni kuwa hatufungi. 

“Lakini pengine, kama tunacheza mchezo wa kujihami na kisha kufanya mashambulizi ya kushtukiza, pengine tutafika mbele ba kufunga mabao mawili au matatyu" Mourinho alisema hayo katika mahojiano na televisheni ya Al-Jazeera, ukionekana ujumbe maridhawa kwa Abramovich aliyekwenda kwenye vyumba vya kuvalia Stamford Bridge baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa ambayo Chelsea ilichapwa 2-1 na Basel Jumatano iliyopita.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog