Saturday, September 21, 2013

Kundi la Wanaume TMK Halisi likiongoza 
na msanii nguli Juna Nature wakilishambulia
 vyema jukwaa usiku huu kwa staili
 yao mapanga shaa shaa,huku mayowe yakipigwa kutoka mashabiki.
Kila shabiki alikuwa na mzuka wake.
Msanii mwingine anaefanya vyema hivi sasa 
katika anga ya muziki wa Bongofleva,Rich Mavoko akiwaimbisha
 mashabiki wake usiku huu,mbele
 ya wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza
 kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,
ndani ya uwanja wa Karume mkoani Mara.
Madansa wa msanii wa muziki wa kizazi kipya,
Shilole wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani
 ya Uwanja wa Karume,ndani ya mji wa 
Musoma mkoani Mara,ambapo tamasha la serengeti fiesta 
2013 likiendelea hivi sasa.
Anajiita tajiri wa Mahaba Cassim Mganga kutoka
 Manzabay akiwaimbisha jukwaani 
wakazi wa mji wa Musoma,wakati
 tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea hivi
 sasa ndani ya uwanja wa Karume.
Mashabiki wakijinafasi kwa raha zao.
 
Kundi la Wanaume TMK likiongozwa na Chege na Temba
 wakilishambulia jukwaa la serengeti fiesta usiku 
huu ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
 
Mkali mwingine wa muziki wa Reggae kutoka kanda ya
 Ziwa,Jita Man akiwakumusha mashabiki wa muziki 
wake enzi hizo,mbele ya wakazi wa mji wa Musoma
 
Anaitwa Godzilla kutoka maskani ya Sala sala,akishusha 
mistari yake live mbele ya mashabiki wake
 waliojitokeza kwenye tamasha la serengeti fiesta usiku huu.
Makamuzi yakiendelea jukwaani usiku
Sehemu ya umati wa watu.
Msanii wa muziki wa bongofleva ambaye kwa 
sasa anafanya vyema kwenye anga hizo,Neylee
 akiimba jukwaani usiku huu wakati wa
 tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea 
usiku huu ndani ya uwanja wa Karume,Musoma mkoani Mara.
Mashabiki wa tamasha la serengeti fiesta
 
 wakifuatilia yanayojiri ndani ya uwanja wa Karume hivi sasa
Sehemu ya umati wa watu ndani ya uwanja wa Karume.
Mwanadada Shilole akionesha umahiri wake 
wa kunengua jukwaani mbele ya maelfu ya 
watazamaji waliojitokeza usiku huu
 kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2013.
Anaitwa Linah Sanga,kutoka nyumba
 ya vipaji THT akiimba jukwaani usiku huu
Watu kibao,kila mmoja akijaichai kivyake
 huku jukwaa likiwaka moto vilivyo kwa 
miondoko ya bandika bandua ya wasanii wanaotumbuiza. 
Wakali wengine wanaokuja kwa kasi
 katika anga bongofleva-hip hop,Stamina na Youngkiller
 wakilishambulia jukwaa kwa kushusha mistari mikavu live.
Shangwe kila kona za mashabiki zimetawala uwanjani hapa.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog