Sunday, January 8, 2017


Mechi za Raundi ya 3 ya Kombe Kongwe kabisa Duniani, FA CUP, zinaanza Leo kwa Mechi moja tu kati ya West Ham na Manchester City itakayochezwa huko London Stadium, Jijini London.
Raundi ya 3, ambayo inaipumzisha EPL, Ligi Kuu England, Wikiendi hii, ndio inayoingiza kwa mara ya kwanza Timu za EPL na zile za Daraja la chini yake, Championship, kushiriki Mashindano haya yaliyotanguliwa na Raundi za Awali zilizohusishwa Timu za Madaraja ya chini.

Jumamosi zipo Mechi 25 na fungua dimba Mchana na huko Old Trafford Jijini Manchester wakati Mabingwa Watetezi Manchester United wakicheza na Timu ya Daraja la Championship Reading ambayo Meneja wake ni Jaap Stam aliewahi kuwa Sentahafu mahiri wa Man United chini ya Meneja Lejendar Sir Alex Ferguson.

JE WAJUA?

-FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.
-Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.

-Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.
-Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.
-Bingwa Mtetezi ni Manchester United.



EMIRATES FA CUP:
Ratiba

Mechi zote kuanza Saa 12 Jioni isipokuwa inapotajwa
Ijumaa Januari 6
22:55 West Ham United v Manchester City

Jumamosi Januari 7
15:30 Manchester United v Reading
Accrington Stanley v Luton Town
Barrow v Rochdale
Birmingham City v Newcastle United
Blackpool v Barnsley
Bolton Wanderers v Crystal Palace
Brentford v Eastleigh
Brighton & Hove Albion v Milton Keynes Dons
Bristol City v Fleetwood Town
Everton v Leicester City
Huddersfield Town v Port Vale
Hull City v Swansea City
Ipswich Town v Lincoln City
Millwall v Bournemouth
Norwich City v Southampton
Queens Park Rangers v Blackburn Rovers
Rotherham United v Oxford United
Stoke City v Wolverhampton Wanderers
Sunderland v Burnley
Sutton United v AFC Wimbledon
Watford v Burton Albion
West Bromwich Albion v Derby County
Wigan Athletic v Nottingham Forest
Wycombe Wanderers v Stourbridge
2030 Preston North End v Arsenal
 

Jumapili Januari 8
1430 Cardiff City v Fulham
1630 Liverpool v Plymouth Argyle
Chelsea v Peterborough United
Middlesbrough v Sheffield Wednesday
1900 Tottenham Hotspur v Aston Villa

Jumatatu Januari 9
2245 Cambridge United v Leeds United

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog