Sunday, January 10, 2016


Msafara wa magari uliokuwa umembeba Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Wachezaji wa Ndani 2015, Mbwana Samata,ulionaswa na Camera ya Globu ya jamii maeneo ya Morocco jana jioni ukitokea hoteli ya Kempinsk baada ya kuzungumza na vyombo vya habari,Msafara huo akiwemo Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye ulipita maeneo kadhaa ya jiji la Dar na kukomea katika kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar,ambako alikutana na kupongezwa na Wadau mbalimbali wa tasnia ya Michezo.Mwanasoka huyo aliwasili juzi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam akitokea Abuja, Nigeria katika hafla ya utoaji tuzo kwa mwanamichezo bora.
PICHA NA MICHUZI JR-MMG.
Baadhi ya Waendesha Boda boda nao hawakuwa na hiyana kuunga mkono mafanikio ya Mbwana Samatta,ambayo yameiletea heshima kubwa nchi yetu.
Msafara wa Mbwana Samatta ukikatiza maeneo ya Morocco
Baadae akawasili viwanja vya Escape One akiwa ameambatana na Waziri Nape Nnauye tayari kwa kukamilisha ratiba nyingine,pia alipata selfie na washabiki wa soka kama uonavyo pichani
Baadae akawasili viwanja vya Escape One akiwa ameambatana na Waziri Nape Nnauye tayari kwa kukamilisha ratiba nyingine,pia alipata selfie na washabiki wa soka kama uonavyo pichani
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini,huku Nyota wetu Mbwana Samatta akiwa amepozi na tuzo yake ya mchezaji bora wa Afrika.
Samatta akipata picha ya pamoja na Waziri Mh.Nape Nnauye.
Wadau wa Soka wakijadiiana jambo,wakati huo Samatta anafanya mahojiano ya hapa na pale na baadhi ya vyombo vya habari
Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba sambamba na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauyewakijumuika pamoja kwenye hafla fupi ya kumpongeza Mbwana Samatta ndani ya kiota cha maraha-Escape One Mikocheni jijini Dar
Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba sambamba na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.Nape na wadau wengine wa soka wakijumuika kwa pamoja kumpongeza Samatta.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog