Sunday, January 10, 2016



Rooney akipiga penati na kumfunga kipa wa Sheffield United.
BAO la Penati ya Dakika ya 93 iliyofungwa na Kepteni Wayne Rooney imewaingiza Manchester United Raundi ya 4 ya FA CUP walipoitungua Timu ya Daraja la chini Sheffield United 1-0 Uwanjani Old Trafford.Penati hiyo ilitolewa katika Dakika ya 92 baada ya Memphis Depay, alieingizwa Kipindi cha Pili na kuleta uhai mkubwa kwenye mashambulizi, kumtambuka John Brayford na kuingia ndani ya Boksi na kuchezewa Rafu na Dean Hammond.
Bao hilo la Rooney lilileta ahueni kubwa kwa Man United kwani walitawala Mechi yote, kwa Asilimia 72 lakini walilenga Shuti 1 tu Golini dhidi ya Timu ya Daraja la chini ambayo iliamua kujihami.
Man United watajua wapinzani wanaofuatia baada ya Droo ya Raundi ya 4 ambayo itafanyika Jumatatu Usiku.

Wayne Rooney akimlalamikia bmwamuzi kuhusu rafu hiyo!Kipindi cha kwanza kilimalizika 0-0
BAADA ya kuanza poa 2016 kwa kuitwanga Swansea City 2-1 kwenye Ligi Kuu England, sasa Manchester United wako tena kwao Old Trafford kucheza Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP na Sheffield United inayocheza Daraja la chini, Ligi 1,ikiwa ni Madaraja Mawili chini ya Ligi Kuu England.
Man United wanaanza kampeni ya kulitwaa Kombe hili ambalo mara ya mwisho walilichukua Mwaka 2004, ikiwa ni mara yao ya 11, na wamepitwa tu na Arsenal waliolitwaa mara 12 baada ya kulibeba mara 2 mfululizo kwa Miaka Miwili iliyopita.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog