Sunday, June 7, 2015


LEO Republic of Ireland na England zilikutana na zilitoka Sare ya 0-0 katika Mechi ya Kirafiki iliyochezwa huko Dublin Nchini Ireland ikiwa ni mara ya kwanza kwa Nchi hizo kukutana huko kwa zaidi ya Miaka 20 baada ya Mechi yao ya mwisho Mwaka 1995 kuvunjika baada ya kutokea fujo za Mashabiki.
Hii Leo Mashabiki walipoa lakini Mechi yenyewe ilipooza kabisa pengine kila Timu ikijilinda kwa ajili ya Mechi zao za Makundi ya EURO 2016 baadae Wiki hii.
Kepteni wa England, Wayne Rooney, akiwania kuvunja Rekodi ya Sir Bobby Charlton ya Bao 49 ya Ufungaji Bora kwa Timu ya England, yeye akiwa na Bao 47, alikosa nafasi moja safi ya kufunga na kwa ujumla alipooza katika uchezaji wake.
Mashabiki wa England wakisubiri kipute hicho mapema leoRaheem sterling akipashaKikosi cha England hii leoTaswira kamiliKikosi cha England kikiwa tayari kupata picha ya pamoja na kuanza kipute cha kirafikiChris Smalling akichuana kuutafuta mpiraPhil JonesRaheem akipatiwa huduma baada ya kuumiaKipute kikiendelea

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog