Saturday, May 30, 2015


download (3) 
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
Kikao cha Kamati ya Utendaji cha Coastal Union ambacho kimeketi
katikati ya wiki hii chini ya Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union,
Steven Mguto kimeazimia kuwaacha baadhi ya wachezaji ambao muda wao
ulikuwa umemalizika huku wengine wakiongezewa mikataba ya kuendelea
kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao.
Kimsingi wachezaji hao wameachwa na sasa wapo huru kutumikia timu
nyengine ambazo zitahitaji huduma zao
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Ofisa Habari wa Coastal
Union,Oscar Assenga amesema
kuwa maamuzi hayo yalifikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya
klabu hiyo ambacho kilifanyika juzi mkoani hapa.
Amesema kuwa kimsingi katika kikao hicho kiliridhia kuwaacha wachezaji
waliomaliza mikataba yao ikiwemo Shabani Kado,Keneth Masumbuko,Yayo
Kato Lutimba, Seleimani Kibuta,Bakari,Razack Khalfani,Itubu Imbem na
Othumani Tamimu.
Aidha amesema kuwa wachezaji wengine ambao klabu imeamua kuwaacha ni
Hussein Sued, Mansour Alawi, Amani Juma, Mohamedi Mtindi na Mohamed
Hassani.
Hata hivyo amesema wachezaji ambao wamemaliza mikataba yao ambao klabu
ipo kwenye mazungumzo nao kwa ajili ya msimu ujao ni Bakari Mtama,Rama
Salim, Godfrey Wambura na Joseph Mahundi.
Wakati huo huo, uongozi wa Coastal Union umewapandisha timu wachezaji
wanne kutoka timu ya vijana kucheza timu ya wakubwa ambao ni Mtenje
Albano, Tumaini Karim, Mohamed Twaha Shekue “Djong”, Fikirini
Suleiman“Mapara”

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog