Friday, February 6, 2015

Jumamosi kesho kwenye Ligi Kuu England, Mechi ya kwanza kabisa ya Ligi huko White Hart Lane, Wenyeji Tottenham wataikaribisha Arsenal kwenye Dabi ya London ya Kaskazini na Mechi hii licha ya kuwa ni Dabi pia ina ushindani wake wa kulilia kuwemo 4 Bora kwani Arsenal wako Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 2 mbele ya Tottenham walio Nafasi ya 6.
Mechi ya mwisho kwa Siku ya Jumamosi ni ile Dabi ya Merseyside Jijini Liverpool Uwanjani Goodison Park ambako Everton wataikaribisha Liverpool.
Katikati ya Dabi hizo mbili zipo Mechi 5 za Ligi zikiwemo ile ya Vinara wa Ligi Chelsea wakiwa Ugenini huko Villa Park kucheza na Aston Villa na Mabingwa Watetezi Man City kuwa Nyumbani Etihad kucheza na Hull City.
Jumapili zipo Mechi 3 za Ligi na mojawapo ni ile ya Uwanjani Upton Park wakati West Ham watakapoikaribisha Man United ambao wako Nafasi ya 3 kwenye Ligi.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Februari 7

15:45 Tottenham vs Arsenal
18:00 Aston Villa vs Chelsea
18:00 Leicester vs Crystal Palace
18:00 Man City vs Hull
18:00 QPR vs Southampton
18:00 Swansea vs Sunderland
20:30 Everton vs Liverpool
Jumapili Februari 8
15:00 Burnley vs West Brom
17:05 Newcastle vs Stoke
19:15 West Ham vs Man United

Jumanne Februari 10
22:45 Arsenal vs Leicester
22:45 Hull vs Aston Villa
22:45 Sunderland vs QPR
23:00 Liverpool vs Tottenham
Jumatano Februari 11
22:45 Chelsea vs Everton
22:45 Man United vs Burnley
22:45 Southampton vs West Ham

22:45 Stoke vs Man City
23:00 Crystal Palace vs Newcastle 

23:00 West Brom vs Swansea

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog