Pichani Kutoka kushoto ni Bella Kombo akiongoza mashambulizi ya jukwaa akipewa sapoti na Digna Mbepera(katikati) na kwa mbaliiiii ni Aneth kushaba.Kama kawaida yetu inapofika mwishoni mwa juma yaani Ijumaa huwa inakuwa ni siku ya furaha na kubadilishana mawazo, kupunguza stress za kazini.....paleee Thai Village Masaki.Kwenye Jukwaa Bendi yako matata na inayotikisa Tanzania na Jiji la Dar Skylight Band wanakuwa wanakupa burudani ya nguvu na iliyoenda shule.Karibu leo kuanzia saa 3 kamili usiku upate zile Afropop, Zouk, Lingala,Sebene, Reggae, Naija Flava na zingine kibao!
Aneth Kushaba AK 47 akizipiga vocal za kutoshaaaa ili kuwapa burudani wapenzi wa Skylight Band ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita.
Bella Kombo akitia madaha yake na swagga kibao ndani ya Thai Village.
Digna Mbepera (Mtoto Mzuri) akiimba kwa hisia kali kuwapa ladha wapenzi wa Skylight band ndani ya Thai Village
Wanamwita tamu ya warembo au Sukari ya warembo si mwingine ni Sam Mapenzi akizipiga zile Vocal lainiii za taratibu kuwapa raha mashabiki wake ndani ya Thai Village
Muziki ni hisia na hapa ndicho anachokifanya Aneth Kushaba hebu mtazame anavyoimba kwa hisia kali na Vitendo ili kuwapa raha mashabiki wake huku akipewa sapoti kwa mbaliiii na Digna Mbepera(katikati) na Bela Kombo wa mwisho kushoto.
Mikono kichwaniii,ahhh ahhhh majembe ya Skylight wakishambulia jukwaa kwa nguvuuuu
Joniko Flower baba ya congo akiongoza kushambulia huku akipewa sapoti na Sony Masamba(katikati) pamoja na Sam Mapenzi.
Mtia ladhaa mahiri wa Skylight akiwa anasahangaa kupata Ukodak kutoka kwa mpiga picha wetu,Huku mpiga drums Idrisa akichunguliaaa kwa mbaliiiii
Huyu jamaa ni muhimu sanaaa ndani ya Sklight Band anaitwa Daudi Tumba,akizipiga Tumba zake lazima ufurahie
0 maoni:
Post a Comment