Wafanyakazi wa Kampuni ya Mafuta ya ENGEN Tanzania leo Novemba 14,2014 wameungana na wafanyakazi wenzao Barani Afrika kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo.Engeni ni Kampuni iliyojikita katika uuzaji wa Mafuta bora ndani na nje ya Tanzania,huku ikiendelea kujivunia kwa Ubora wake.Pichani ni Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni hiyo ya Engen hapa nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya jengo lao Kurasini jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya ENGEN Tanzania,Mubita Akapelwa (wa pili kulia) akikata keki wakati wa Kusherehekea Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo,iliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Ofisi za Kampuni hiyo,Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Shaaban Kayungilo.
Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Shaaban Kayungilo akichua kipande cha Keki iliyokatwa vyema na Dada Jullieth Lwato (alieshika sahani) wakati wa Kusherehekea Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo,iliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Ofisi za Kampuni hiyo,Jijini Dar es Salaam.
0 maoni:
Post a Comment