Dakika
ya 87 Daley Blind aliisawazishia bao Man United na kufanya 2-2 na
kuwaokoa Man United huko Hawthorns kwa sare hiyo ambayo aikuleta
mabadiliko kwa timu zote mbili licha ya kugawana pointi moja. Sare hii
inambakisha Man United nafasi ya 6 na pointi zake 12 huku West Brom
Albion wakibaki nafasi ya 15 na pointi zao 9. Dakika
ya 66 kipindi cha pili Saido Berahino aliwachomoka mabeki wa United na
kuwafunga bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya United baada ya
kutanguliziwa pasi na Chris Brunt.Kipindi
cha pili dakika ya 48 Marouane Fellaini aliwasawazishia bao safi Man
United baada ya kupata krosi kutoka kwa Di Maria na Fellaini aliingia
ndani ya Dimba akitokea benchi kuchukua nafasi ya Ander Herrera katika
kipindi cha pili dakika ya 46.Fellaini akishangilia bao lakeStéphane Sessegnon akiruka juu kwa kushangilia baada ya kufunga bao la mapema dakika ya nane. Mpaka
dakiks 45 zinakatika za kipindi cha kwanza West Brom Albion ndio
walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Manchester United.Stéphane Sessegnon akishangilia bao lake mapema kipindi cha kwanza baada ya kuweka 1-0 dhidi ya Man United.Dakika
ya 8 kipindi cha kwanza West Brom wanafanya shambulizi kali na kupata
bao la kuongoza kupitia kwa Stéphane Sessegnon baada ya kupata pasi
safi kutoka kwa Andre Wisdom.
0 maoni:
Post a Comment