Akiongea Jana na Wanahabari kuhusu Mechi hiyo, Meneja huyo alisema hivi sasa ni Wachezaji Wanne tu ambao ndio Majeruhi na Ijumaa aliweza kuwa na Wachezaji wengi wa Timu ya Kwanza kiasi cha kutolazimika kuchukua Wachezaji wa Timu ya Pili ili kuja kuongeza idadi kwenye Mazoezi.Louis van Gaal amesema wapo kwenye hali njema wakati anaitayarisha Timu yake Manchester United Jumatatu Usiku kwenda huko The Hawthorns kuivaa West Bromwich Albion kwenye Ligi Kuu England.
Akiongea Jana na Wanahabari kuhusu Mechi hiyo, Meneja huyo alisema hivi sasa ni Wachezaji Wanne tu ambao ndio Majeruhi na Ijumaa aliweza kuwa na Wachezaji wengi wa Timu ya Kwanza kiasi cha kutolazimika kuchukua Wachezaji wa Timu ya Pili ili kuja kuongeza idadi kwenye Mazoezi.
Alieleza: “Asubuhi hii hatukuhitaji Wachezaji wa Timu ya Pili na hii ni habari njema. Nina furaha hatuna Majeruhi zaidi kutoka Mechi za Kimataifa. Tupo hali njema. Wapo Wachezaji wanaoendelea kupona na tutaangalia hadi Jumatatu Kikosi kitakuwa kipi. Hivi sasa tuna Wachezaji Wanne tu majeruhi. Hii ni safi.”
Wachezaji ambao bado ni Majeruhi ni Mabeki Jonny Evans na Paddy McNair na Mawinga Jesse Lingard na Antonio Valencia lakini pia Man United itamkosa Nahodha Wayne Rooney ambae anatumikia Kifungo chake cha Mechi 3 kwa Kadi Nyekundu.
LEO Jumatatu, Van Gaal anasaka ushindi wake wa kwanza wa Ugenini dhidi ya WBA ambayo imeshinda Mechi zao mbili za Nyumbani zilizopita dhidi ya Burnley na Hull City.
Van Gaal ameeleza: “Nadhani WBA ni Timu ngumu kuifunga hasa Nyumbani kwao. Wanacheza Pasi ndefu lakini pia wanazuia nafasi. Ni Wapinzani hatari. Lakini kila Mpinzani Ligi Kuu ni mgumu. Tunataka tuanze na ushindi baada ya mapumziko ya Mechi za Kimataifa.”
0 maoni:
Post a Comment