Mmoja wa askari waliokuwa wamepangwa katika suala zima la kusimamia usalama ndani ya tamasha la Fiesta 2014 akihakikisha usalama wa kutosha unakuwepo katika eneo hilo,na watazamaji wanapata burudani iliyokusudiwa kutoka kwa wasanii mbalimbali waliotumbuiza usiku wa kuamkia leo katika tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
Shaa na madansa wake wakilishambulia jukwaa.
Pichani kulia ni Msanii kutoka nchini Nigeria ajulikanae kwa jina la Kisanii Davido sambamba na Diamond Platnum kwa pamoja wakilishambulia jukwaa la fiesta 2014 usiku wa kuamkia leo.
Msanii kutoka THT,Barnaba akiimba wimbo wake wa Wahalade sambamba na madansa wake kwenye jukwaa la fiesta 2014,katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
Sehemu ya umati wa watu waliokuwa wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
Ilikuwa ni shoo moja nzuri kutoka nyumba ya vipaji ya THT
Pichani msanii Linah (nyeupe) akiwa na skwadi lake mara baada kumaliza kulishambulia jukwaa kwa pamoja.
Anaitwa Ally kiba ambaye inaelezwa kutoka kwa mashabiki kuwa alifanyo shoo nzuri na iliyowavutia,na kuthibitisha uwezo wake kuwa ni kweli amerejea kwenye kiti chake cha usanii.
Msanii kutoka nchini Marekani Clifford Haris a.k.a T.I akilishambulia jukwaa la Fiesta vilivyo
Msanii kutoka nchini Marekani T.I akiwaimbisha mashabiki wake
PICHA NA MICHUZI JR,
0 maoni:
Post a Comment