Monday, September 1, 2014


FalcaoManchester United imekubaliana na AS Monaco ya France kumsaini Straika wa Colombia Radamel Falcao kwa Mkopo na wakati huo huo Straika wao Javier Hernandez anahamia Real Madrid ya Spain pia wa Mkopo.
Falcao anatarajiwa kuwasili Jijini Manchester kupimwa afya yake na tayari Chicharito nae yuko huko Madrid kupimwa afya.
Falcao alijiunga na AS Monaco Mei 2013 kwa Dau la Pauni Milioni 50 kutoka Atletico Madrid na kufunga Bao 11 katika Mechi alizoichezea.

Msimu huu Falcao amefunga Bao 2 katika Mechi 3.
Dili ya Falcao kwenda Man United pia ina makubaliano kuwa wanaweza kumnunua moja kwa moja kwa Dau la Pauni Milioni 43.5.

Mwezi Januari Falcao aliumia vibaya Goti lake na kumfanya alikose Kombe la Dunia.
Meneja wa Manchester United Louis Van Gaal tayari ameshawasaini Luke Shaw, Marcos Rojo, Ander Herrera na Angel Di Maria huku Mchezaji wa Netherlands Daley Blind akiwa njiani kujiunga.

Javier Hernandez ni dole tuu!! Baada ya kutua Real! mambo super!

Hernandez anaenda Real kuongeza ujuzi akitokea  Manchester United kwa mkopo!

Hernandez alikuwa akisugua benchi pale United na sasa ameenda Real kuona kama namba ya kudumu atapata ya kikosi cha kwanza.

Hernandez alipofika Real na tayari kwa kutambulishwa Klabuni hapo jana jumatatu

Hernandez kuonesha kiwango chake hapo  Real Madrid

Hernandez akitabulishwa na atavaa jezi no. 14

Hernandez  akitabasamu mbele ya makombe  Bernabeu

Chicharito'akiwa na  Perez  Bernabeu

Hernandez tayari kwa kuichezea  Real Madrid baada ya vipimo kwenda safi jana jumatatu!

Akiwamwagia wino mashabiki!

Safi! Chicharito amefurahia kutua Real

Javier Hernandez alipokuwa na Daktari

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog