Monday, September 1, 2014



Wachezaji Liverpool wakishangilia ushindi
Ligi kuu ya England ambayo imendelea jumapili kwa timu sita kujitupa uwanjani katika michezo mitatu.
Katika mechi ya kwanza Meneja wa Liverpool Brenden Rodgers alitimiza mechi yake 100 tangu aichukue usukani wa kuifundisha liverpool kwa kushuhudia timu yake ikiisambaratisha Tottenham Hotspur kwa jumla ya magoli 3 kwa 0.
Liverpool walianza kuonja ushindi katika dakika ya 8 kwa goli lililofungwa na Raheem Sterling.
Baadae Nahodha wa timu hiyo Steven Gerrald katika dakika 49 akafunga goli la pili kwa mkwaju wa penalty baada ya Joe Alllen kudondoshwa kwenye kisanduku cha 18 kwenye goli la Tottenham.
Goli la tatu la Liverpool lilifungwa na Alberto Moreno Perez baada ya kuwatoka mabeki wa Tottenham na kufunga goli la tatu katika dakika 60.
Hadi mechi hiyo inamalizika Tottenham 0 Liverpool 3
Nayo Aston Villa ambao waliiadhibu Hull City magoli 2 na Hull City 1.
Aston Villa ndio walioanza kufunga goli lililofungw Gabriel Agbonlahor katika dakika ya 14.
Aston villa wakaandika goli la pili ambalo lilifungwa na Andreas Weimann katika dakika ya 36.
Nao Hull City walipata goli moja la kufutia machozi lililofungwa na Nikica Jelavic.
Mechi ya mwisho iliyomalizika usiku ilikuwa ni kati ya Leicester City na Arsenal na matokeo ni kwamba Leicester goli 1 na Arsenal wamepata goli 1.
Kwa matokeo hayo sasa Chelsea ndio wanaoongoza msimamo wa ligi ya England kwa pointi 9 wakifuatiwa na Swansea iliyoshika nafasi ya pili nayo ikiwa na pointi 9 ila ikiwa na toufuti ya magoli Aston Villa ya tatu, Manchester City ya nne, Liverpool ya tano, Tottenham ya sita, Arsenal ya saba na Manchester United ikishika nafasi ya kumi na nne.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog