Beki wa kati wa klabu ya Arsenal
Laurent Koscielny ameondolewa katika kikosi chake cha cha timu ya taifa kwa
sababubu ya majeraha ya kichwa yaliyompata baada ya hapo jana kugangana na
mchezaji wa klabu ya Leicester City,Jeffrey Schlupp katika mchezo uliofanyika
dimani King Power na timu zote kutoka sare ya goli 1-1.
Koscienly alipata jeraha hilo mnamo dakika ya 26 ya mtanange huo ambao nafasi yake ililazimika kuchukuliwa na Calum Chambers Taarifa katoka shirikisho la soka nchini Ufaransa zimedhibitisha kuwa beki huyo kwa sasa hayupo katika hesabu ya wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa kinachotarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki siku za karibuni kati Hispania na Serbia.
Nafasi ya Koscienly kwa sasa katika
kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa inaonekana kuchukuliwa na beki anayekipiga
kunako klabu ya Barcelona Jeremy Mathieu.
Mathieu, amejiunga na Wakatalunya
msimu huu akitokea Valencia na amekwisha fanikiwa kucheza michezo miwili ya
kimataifa.
Kitengo cha utabibu ya klabu ya Arsenal kimesema kinaendelea na uchunguzi wa jeraha hilo kisha watasema rasmi ni kwa muda gani beki huyo atakuwa nje ya dimba akiuguza jeraha lake.
0 maoni:
Post a Comment