MCHEZAJI wa Simba
Willium Lucian ‘Gallas’ amebadilisha nafasi katika kikosi cha Simba kutoka beki
wa kulia alikokuwa akicheza awali na kupelekwa kucheza kama kiungo mkabaji
kikosini hapo.
Kocha wa Simba, Mzambia
Patrick Phiri ameamua kumbadilisha Gallas na kumpeleka katikati baada ya
kugundua kuwa beki huyo mbali na uwezo wa kucheza kama beki wa kulia pia
anaweza kucheza kama beki wa kati ama kiungo mkabaji.
Mabadiliko hayo
yamechagizwa zaidi na kuumia kwa kiungo Jonas Mkude, ambaye ameiacha nafasi
hiyo ya kiungo chini ya Mrundi Pierre Kwizera pekee. Said Ndemla na Abdallah
Seseme ambao wanaweza kucheza katika nafasi hiyo si wazuri katika kukaba jambo
lilimfanya Phiri kufanya maamuzi hayo.
Mkude aliumia alipokuwa
na Taifa Stars nchini Botswana mapema Julai mwaka huu na kulazimika kukaa nje
kwa zaidi ya miezi miwili. Taarifa kutoka kwa daktari wa Simba, Yassin Gembe ni
kwamba Mkude atarejea rasmi uwanjani Oktoba 12.
“Ni kweli nimeamua
kumpeleka Gallas katikati, ni mzuri anapocheza hapo kwani anajua kukaba lakini
pia anaweza kucheza kama beki wa pembeni na kati, ni mchezaji mzuri,” alisema
Phiri.
Katika mchezo dhidi ya
Gor Mahia Jumamosi iliyopita, Gallas alichezeshwa katika nafasi hiyo ya kiungo
na kucheza kwa ustadi kabla ya kufanyiwa mabadiliko katika kipindi cha pili.
0 maoni:
Post a Comment