Issa Rashid (kulia)
BEKI wa Simba Issa
Rashid ‘Baba Ubaya’ atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa wiki mbili baada ya
kuumia nyama za paja kwenye moja ya mazoezi ya klabu hiyo, daktari wa Simba,
Yassin Gembe amethibitisha.
Mbali na beki huyo
straika Elius Maguli alilazimika kupumzishwa kufanya mazoezi na wachezaji
wengine baada ya kuugua Malaria ambapo mpaka jana Jumatano mchana haikufahamika
mara moja kuwa angerejea kuendelea na programu hizo siku gani.
Gembe alisema baada ya
kwenda kumfanyia vipimo Jumatatu ya wiki hii, Baba Ubaya alishauriwa kukaa nje
kwa muda wa wiki mbili wakati Maguli alipumzisha juzi Jumanne kufanya mazoezi
na wachezaji wenzake kutokana na kusumbuliwa na Malaria.
“Baba Ubaya atalazimika
kukaa nje kwa wiki mbili kuanzia leo (Jumanne) baada ya kugundulika kuwa
majeraha yake ya nyama za paja si madogo kama tulivyodhani mwanzo,” alisema
Gembe
Majeraha hayo yatamfanya
Baba Ubaya kuukosa mchezo wa ufunguzi wa Ligi kati ya Simba na Coastal Union
utakaochezwa Jumapili ya Septemba 21.
Chanzo: Mwanaspoti
0 maoni:
Post a Comment