Manchester United walimuuza Danny Welbeck kwa wapinzani wao wakubwa Arsenal baada ya kumsaini Radamel Falcao.
GARY Neville ameishutumu sera ya usajili
ya Manchester United baada ya kudai kuwa alishangazwa na kitendo cha
kumuuza Danny Welbeck kwa paundi milioni 16 tu.
United walitumia fedha nyingi majira ya kiangazi kwa kumsajili Falcao, Angel di Maria, Daley Blind, Ander Herrera, Luke Shaw na Marco Rojo.
Neville alisema: "Sikutarajia kama United wangefanya biashara kama hiyo, nalidhani wangefanya zaidi ya hapo"
"Siwezi kusema sana, wiki iliyopita
nilifanya kazi na Danny Welbeck (akiwa na England), hakika ni ajabu.
Nakiri wazi kuwa kumuuza Danny Welbeck ni ajabu, lakini ni kwa upande
wangu".
"Kwa pesa zote walizotumia majira ya kiangazi, kuna mabeki wa kushoto na kulia walionunuliwa kwa paundi milioni 14, 16, 16?
"Arsenal walimpaje Welbeck kwa paundi
milioni 16? Sielewi. Wamewasaidia wapinzani kwasababu Arsenal watakuwa
wanapambana kusaka nafasi nne za juu"
"Napata shida kupata logiki, lakini sielewi, inashangaza kwa namna moja ama nyingine".
"Falcao aliingia pale, ilimshangaza kila mtu. Inaingiaje kwenye timu, sijui. Tayari walikuwa na Rooney, Di Maria, Robin van Persie, Falcao, Herrera, Januzaj na Mata katika timu.
Arsene Wenger alimsajili Danny Welbeck baada ya mshambuliaji wake chaguo la kwanza Olivier Giroud kuumia
Radamel Falcao alijiunga Manchester United kwa mkopo wa Muda mrefu.
Neville aliendelea kudai kuwa United imelipa hela nyingi zaidi kwa wachezaji baada ya kushika nafasi ya saba msimu uliopita.
0 maoni:
Post a Comment