Wachezaji
wa Man utd wakiwa mazoezini pamoja na kocha mkuu David Moyes. Mazoezi
haya ni ya mwisho mwisho kabla ya kukutana na Olympiacos usiku wa leo.
United itaingia uwanjani ikiwa nyuma kwa magoli 2-0 baada ya kukubali
kipigo kwenye mechi ya awali nyumbani kwa Olympiacos. Ili kupita kwenda
hatua inayofuata United wanatakiwa kushinda magoli 3-0 jambo ambalo
linawezekana kwa timu kama Manchester United. Washabiki na wachambuzi
wengi wanakubali kuwa United ya sasa sio kama ya zamani, lakini
wanaamini kuwa wachezaji waliopo kama kocha atachagua kikosi kizuri basi
Olympiacos lazima walie. Uzito wa mechi ya leo unaongezeka zaidi baada
ya taarifa kuanza kuzagaa kuwa kibarua cha kocha David Moyes kitakua
kwenye joto kali kama United watashindwa kusongambele kwenye michuano
hii. Hali hii inakuja kutokana na ukweli kwamba Man utd wamepoteza
nafasi ya kushinda vikombe vyote ndani ya England na Uefa champions
ndiyo kombe pekee lililobakia kwa Moyes kuonesha muujiza. Usikose
kuangalia mechi ya leo saa nne dk 45 usiku.
0 maoni:
Post a Comment