Wednesday, March 19, 2014




Didier Drogba husakata soka yake Galatasaray

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho anaamini kuwa gwiji wa soka Didier Drogba angali mmoja wa washambuliaji bora zaidi duniani.
Drogba anayesakata soka yake na klabu ya Galatasaray na ambaye aliondoka Stamford Bridge Juni mwaka 2012, leo anarejea kwa mkondo wa pili wa vilabu vilivyosalia katika kombe la klabu Bingwa Ulaya kufuzu michunao hiyo.
Ikiwa Drogba ataingiza bao huenda asisherehekee uwanjani Stamford Bridge
Mourinho alisema Drogba angali na makali aliyokuwa nayo alipokuwa miaka 26 , na hakuna anayeweza kuwa katika hali hiyo akiwa na umri wa miaka 36. Lakini ni mshambulizi hodari sana.
Drogba amesema huenda hatasherehekea ikiwa ataingiza bao dhidi ya wachezaji wenzake wa zamani.
Mchezaji huyo kutoka Ivory Coast aliingiza mabao 157 katika mechi 342 wakati alipokuwa anachezea Chelsea kwa miaka minane.
Mourinho, aliyemsajili Drogba katika klabu ya Chelsea kutoka Marseille mnamo mwaka 2004, alishangiliwa sana aliporejea katika klabu hiyo mwezi Agosti mwaka jana
baada ya kuwa nje kwa karibu miaka sita.

Anatumai kuwa Drogba atang'aa katika mechi ya leo usiku.
Chelsea itakuwa klabu ya kwanza, kufika robo fainali ya michuano hiyo ikiwa watashinda leo usiku dhidi ya Galatasaray na duru zinasema kuwa Mourinho yuko ngangari

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog