Monday, January 20, 2014




Wafanyakazi wa shirika la Msalaba mwekundu wakiwasaidia waliojeruhiwa C.A.R
Kumekuwa na machafuko zaidi katika Jamhuri ya Afrika ya kati, siku moja kabla ya baraza la mpito kumchagua rais mpya wa nchi hiyo.
Mwandishi wa BBC katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui, ameona miili ya Waislamu wawili iliyoteketezwa moto.
Wapiganaji wa Wakristo wamesema waliwaua watu hao kulipiza kisasi mauaji ya awali ya muumini mmoja wa dini ya Kikristo.
Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu, ICRC, inasema machafuko mapya ya kidini yalizuka siku ya Jumapili Kaskazini na Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.
Muungano wa Ulaya unatarajiwa leo kuidhinisha kutumwa kwa kikosi cha wanajeshi wa Ulaya kujiunga na wale wa Afrika na Ufaransa walio nchini humo.
Mauaji hayo yanasadikiwa kuchochea machafuko mapya mjini Bangui.

Mapigano ya kidini

Wapiganaji wa Kikristo nchini C.A.R
Mtu wa kwanza aliyeuawa anasemkana kuwa ni Mkristo mmoja aliyejulikana vyema kutoka mtaa unaoitwa Sangoh.
Waliomvamia walimlenga kwa sababu za kushirikiana na Waislamu wa mtaa uitwao District five, ambao wakaazi wake wamelaumiwa kufanya mashambulizi dhidi ya mitaa jirani ya Wakristo.
Mwili huo ulichomwa wakati waandishi walipokuwa wanawasili katika eneo hilo.
Mara vurugu zikaanza tena, na mwanamme mmoja Muislamu aliyekuwa ndani ya taxi akavamiwa, na kushambuliwa hadi kufa.
Pia yeye akachomwa moto huku wavamizi hao wakiwasaka Waislamu wengine.
Hayo yote yamefanyika licha ya Kuwepo kwa kikosi cha wanajeshi wa nchi za kiafrika ambao walishindwa kuzuia ukatili huo.
Wakati huo huo wanachama 135 wa baraza la kitaifa la mpito wanatarajiwa kumchagua rais mpya wa mpito, baadaye Jumatatu.
Waandishi wa habari wanasema kiongozi huyo mpya atakuwa na kibarua kigumu kurejesha hali ya utulivu na utawala wa sheria nchini humo.


0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog