Wednesday, January 15, 2014




 

Mchezaji mkongwe wa AC MILAN na timu ya taifa ya uholanzi, Clarence Seedorf, Amekuwa Meneja mpya wa AC Milan ya Italy baada kutangaza kustaafu kucheza Soka.
Seedorf, Miaka 37, ambae aliichezea Klabu hiyo Kigogo ya Italy kati ya Mwaka 2002 hadi 2012, anambadili Massimiliano Allegri alietimuliwa kazi Jumatatu.

Clarence Seedorf:

-Umri: Miaka 37
-Uraia: Netherlands
-Klabu: Ajax (1992-95); Sampdoria (1995-96); Real Madrid (1996-2000); Inter Milan (2000-02); AC Milan (2002-2012); Botafogo (2012-2014)
-Holland: Mechi 87

Tearful: Clarence Seedorf (right) is embraced by his former coach from Botafogo, Eduardo Hungaro, as he says goodbye to his Brazilian club
Clarence Seedorf akiwa na kocha wa zamani wa Botafogo, Eduardo Hungaro na amemtakia mafanikio mema ya mwaka 2014 huko Milan baada ya Milan kumlima shoka kocha wake.

Farewell: Clarence Seedorf (left) says goodbye to his teammates from the Brazilian club Botafogo in Rio de Janeiro
Clarence Seedorf akiwaaga wenzie wabrazil katika club ya Botafogo huko Rio de Janeiro-Brazil.
Msimu huu, kwenye Serie A, AC Milan wanasuasua kwa kushinda Mechi 5 tu kati ya 19 na wako Pointi 30 nyuma ya Vinara Juventus.
Jumapili iliyopita, AC Milan ilichapwa Bao 4-3 na Sassuolo.
Akiwa na AC Milan, Seedorf alicheza Mechi zaidi ya 400 na kutwaa Ubingwa wa Serie A mara 2 na UEFA CHAMPIONS LIGI mara 2.
Pia, Seedorf alikuwa Mchezaji wa Kwanza kutwaa UEFA CHAMPIONS LIGI mara 3 na Klabu 3 tofauti baada kushinda akiwa na Ajax Mwaka 1995, Real Madrid 1998 na AC Milan, Miaka ya 2003 na 2007.
Seedorf, ambae pia alizichezea Klabu za Inter Milan na Sampdoria, baada kuondoka AC Milan alijiunga na Klabu ya Brazil, Botafogo, Mwaka 2012.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog