Wednesday, January 15, 2014

MICHUANO ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya bara hili, CHAN inaendelea kushika kasi ambapo wenyeji Afrika Kusini wanatarajia kutupa karata yao ya pili kwa kupambana na Mali katika mchezo wa kundi A jioni hii.Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana itakuwa inatafuta ushindi ili kuendelea kuongoza kundi hilo baada ya kuwagaragaza majirani zao Msumbiji kwa mabao 3-1 katika mchezo wa ufunguzi. Mbali na hilo Bafana Bafana itahitaji ushindi huo ili kupunguza presha katika mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi ambapo watakutana na Nigeria walichapwa na Mali kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza. Mechi nyingine ya kundi hilo itazikutanisha Nigeria na Msumbiji ambazo zitachezwa baada ya mechi ya kwanza jijini Cape Town.Kikosi cha Bafana Bafana

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog