Mbunge wa Iramba Magharibi, mh. Mwigulu Nchemba leo asubuhi aliomba mwongozo wa Spika wa bunge akimtuhumu Mh. Mbowe kwamba amekuwa akitumia madaraka yake vibaya kwa kuchanganya mapenzi na kazi, hali inayolichafua bunge la Tanzania katika tawsira za kimataifa.....
Mwigulu ameliambia bunge kuwa , Mbowe alipiga simu kutaka kusitishwa kwa safari ya mbunge wa viti maalumu Chadema mkoa wa Arusha Joyce Mukya (inasemekana ni mpenzi wake) aliyekuwa ametumwa na bunge kwenda Dominica Republic kwa ajili ya kazi za bunge....
Kwa
mujibu wa Mwigulu, Joyce akiwa huko alipigiwa simu na Mbowe
akimtaka akatishe safari hiyo na badala yake aelekee Dubai kula
bata na Mbowe, kitu ambacho amedai kuwa ni matumizi mabaya ya
pesa za bunge ( posho) ...
Aidha , Mwigulu ameliomba bunge lifanye uchunguzi kuhusu posho zilizotolewa kwa mbunge huyo ambaye alikatisha safari halali ya bunge na kumfuata mpenzi wake ( Mbowe ) Dubai.
0 maoni:
Post a Comment