Monday, November 25, 2013

http://www.theclicktz.com/
Ndugu zangu,
Siasa ni burudani pia. Tangu jana niliposikia habari za wawili hawa; Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo kupigwa kikumbo kizito ndani ya Chadema, basi, nikajisemea, kuwa habari kubwa leo Jumamosi ni za waheshimiwa hawa wawili.
Naam, Zitto Kabwe ni habari kubwa. Maana, hata jana jioni Mtangazaji wa Redio Ujerumani alinipigia simu kutaka maoni yangu.
Tafsiri isiyo rasmi ni kuwa, Zitto Kabwe ameondoshwa Chadema, walau kwa sasa.
Na Wajomba zangu Wazaramo mtu akiondoka husema, 'fulani kachola'. Kwamba kaondoka. Na mtu huyo akirudi, basi, husema, ' fulani kabwela'. Kwamba amerudi.(P.T)
Na ya Zitto Kabwe na Chadema wala hayana upya katika siasa. Yamenifanya nisome tena historia. Nimeyakuta vitabuni yenye kufanana, wala sisemi kwenye vitabu gani na wala siyasimulii leo. Yasije yakaathiri ' mwenendo wa harakati za wadadisi wa mambo!'
Na wanasiasa wana maisha yao ya kisiasa. Siku zote maisha ya kisiasa yanaendelea. Na mwanasiasa huyaishi maisha ya kisiasa. Yawe ni shwari au yenye mawimbi. Akiacha kuyaishi, basi, hufa kisiasa.
Mwanasiasa ni kama samaki kwenye lambo. Nje ya lambo samaki hana uhai. Na samaki anapotolewa nje ya lambo ana mawili tu ya kuchagua; kupambana kurudi lamboni au kufa.
Na aliyeondoka kwenye safari ya kisiasa anaweza kurudi au kupotea njiani.
Na kama leo imeandikiwa ' Zitto Ka-Chola' na tusubiri basi kusoma kama itaandikwa; ' Zitto- Ka-Bwela'!
Ingawa swali litabaki; Zitto Ka-bwe-laje?
Naam, Zitto amerudi vipi?
Maggid Mjengwa.
Iringa.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog