Sunday, July 28, 2013

 Chokochoko za Nduli Iddi Amin Dada, kuichokoza Tanzania hadi kupelekea kuanza kwa vita iliyomfaya aikimbie nchi yake mwaka 1978, ulikuwa ni Mto huu wa Kagera, ambapo alikuwa akitaka mto huu ndiyo uwe mpaka halisi unaotenganisha nchi yake ya Uganda na Tanzania. Jambo hilo lilimkasilisha sana Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, aliyeamua kumuadabisha baada ya yeye kutangaza kwa kejeli kubwa kuwa anauwezo wa kuisambaratisha Tanzania, na kwamba alikuwa na uwezo wa kuwa anapata chakula cha mchana Jijini Dar es Salaam huku akiendelea kushambulia.
 Baada ya Idd Amin kuona Majeshi ya Tanzania tayari yameshajiandaa kwa vita na yakizidi kusonga mbele kuelekea nchini kwake, aliamua kuvunja Daraja la mto Kagera kwa bomu, pamoja na Kanisa hili la Kyaka, lililopo pembezoni kabisa mwa Mto huo, ambalo kwa sasa limebaki kuwa sehemu ya kumbukumbu ya Vita hiyo iliyosababisha vifo vya askari wetu Mashujaa kadhaa, ambao hukumbukwa kila Julai 25, kila mwaka.
 Sehemu ya Makaburi ya Mashujaa wa Tanzania, waliokuwa mstari wa mbele kuitetea Tanzania, kuhakikisha wanamuondoa Nduli Idd Amini, hapa wakiwa wamelazwa katika makaburi yaliyopo Kambi ya Kaboya Mkoani Kagera.
 Mnara wa Mashujaa, wenye majina ya Askari wetu Mashujaa waliojitolea kuitetea Tanzania.
 Hii ni sehemu ya maonyesho iliyobaki kuwa kumbukumbu ya Vita hiyo kwa vizazi na vizazi. 
 Hii ni Injini ya Ndege ya Jeshi la Nduli Iddi Amini aliyekuwa Rais wa Uganda, iliyolipuliwa kabla ya kushambulia Kanisa la Kyaka mwaka 1978. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

 Hii ni Gari aina ya Jeep iliyokuwa ikitumiwa na Majeshi ya Nduli Iddi Amini wa Uganda, iliyokuwa ikitumika kufanya Doria.
 Hii ni mabaki ya gari aina ya Unimog iliyokuwa ikitumiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika vita hiyo ya mwaka 1978.
 Hii ni gari aina ya Jeep, pia ilikuwa ikitumiwa na Jeshi la Nduli Iddi Amini.
 Hii ni Gari aina ya Benzi, lililokuwa likitumiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania, wakati wa Vita hiyo.
 Hii ni gari aina ya Unimog iliyokuwa ikitumiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Vita ya mwaka 1979.
 Hii ni Rada ya Kirusi iliyokuwa ikitumiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania, wakati wa Vita hiyo kuanzia mwaka 1978-79.
 Hili ni moja kati ya Madaraja yaliyokuwa yakitumika kuvusha Askari baada ya Daraja la Mto Kagera la Kyaka kulipuliwa na Jeshi la Uganda.
 Hili ni Bomu la Ndege ya Jeshi la Nduli Iddi Amini, lililolipuliwa na Majeshi ya Tanzania. 
 Viongozi wakitembelea kujionea Makaburi ya Mashujaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, iliyofanyika katika Kambi ya Kaboya mkoani Kagera, Julai 25, mwaka huu.
 Mmoja wa Askari akiwa kazini kunasa matukio siku hiyo maalum ya Kitaifa.
 Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza viongozi wenzake kutembelea na kuona sehemu ya vifaa vya kumbukumbu ya vita hiyo. Hapa wakiangalia Injini ya iliyokuwa Ndege ya Jeshi la Amini, iliyolipuliwa na jeshi la Tanzania kabla ya kushambulia Kanisa la Kyaka.
 Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na mmoja kati ya Askari Wastaafu Mashujaa, waliopigana Vita. Huyu ni Mzee Andrea Mtangi (89), aliyepigana Vita kuu ya pili Dunia.
 
Mzee Andrea Mtangi (89) (kushoto) na mwenzake wakitoka eneo la tukio baada ya sherehe hizo.
 Mmoja kati ya wazee Mashujaa wastaafu akiwa na vyeo vyake alivyostaafu navyo.
 
 
 Sehemu ya wakazi wa mkoani Kagera waliojitokeza kushuhudia maadhimisho hayo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog