wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limetangaza Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga utafanyika tarehe 05, Julai 2015.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi
ya TFF, Wakili Melchesedek Lutema ametoa ratiba ya mchakato mzima wa
uchaguzi huo, ambapo tarehe 21-22 Mei mwaka huu zitatangazwa nafasi zote
zinazogombewa.
Kwa mujibu wa kalenda hiyo ya
Uchaguzi, tarehe 23-30, Mei 2015 itakua ni kipindi cha uchukuaji fomu
kwa wagombea wote na kuzirudisha, wakati Juni Mosi mpaka Juni 04, 2015
ni kipindi cha mchujo wa awali kwa wagombea.
Juni 05, 2015 Kamati ya Uchaguzi
itatoa orodha ya awali ya wagombea, Juni 7-9, 2015 itakua ni kipindi cha
kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea, na Juni 10-11 ni kupitia
mapingamizi yote.
Julai 02 -04, 2015 ni muda wa kampeni kwa wagombea wote na uchaguzi mkuu utafanyika tarehe 05, Julai 2015.
Ratiba kamili ya mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Coastal Union imeambatanishwa.
0 maoni:
Post a Comment