Huko Manchester United, Meneja wao louis van Gaal alijizolea sifa kemkem kwa spichi yake murua iliyofurahisha na kuhamasisha na kushangiliwa mno Ukumbini na kujizolea sifa kubwa katika Mitandao ya Jamii.
Katika Hafla hiyo, kwa Misimu miwili mfululizo, Kipa David De Gea alitwaa Tuzo mbili za Mchezaji Bora wa Wachezaji, inayochaguliwa na Wachezaji wenyewe, na ile ya Mchezaji Bora wa Washabiki, inayopigiwa Kura na Mashabiki.
Hivi sasa Kipa De Gea amegubikwa na uvumi wa kutaka kuhamia Real Madrid licha ya kupewa Mkataba mpya ulioboreshwa ambao hajausaini.
Tuzo za Goli Bora la Msimu ilikwenda kwa Juan Mata kwa Goli lake la pili dhidi ya Liverpool.
Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana ilichukuliwa na Mbrazil Andreas Pereira.
Huko Liverpool, Winga machachari, Raheem Sterling alizomewa wakati akipanda Jukwaani kupokea Tuzo yake ya Mchezaji Bora Kijana wa Msimu.
Sterling alipokewa kwa shangwe iliyobadilika na kuja kuzomewa na miluzi ikiwa ni ishara ya Washabiki kuchukizwa kwa kukataa kwake kusaini Mkataba mpya akidai kuhama Klabu hiyo.
Lakini Mbrazil Philippe Coutinho ndie alieibuka Shujaa wa Liverpool kwa kutwaa Tuzo 3 za Mchezaji Bora wa Msimu, Goli Bora la Msimu, lile la Shuti la mbali dhidi ya Southampton na Tuzo ya Tukio la Uchezaji wa Ustadi.
Meneja Van Gaal akwa na mshindi tuzo mara mbili David de Gea (Tuzo mbili za Mchezaji Bora wa Wachezaji)
Van Gaal, De Gea pamoja na Steve Cross wakiwa na Kombe kama Tuzo ya Sir Matt Busby mchezaji bora wa mwaka.
0 maoni:
Post a Comment