Tuesday, May 12, 2015

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo leo asubuhi nyumbani kwa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye John Nyerere kilichotokea hivi karibuni.Aliyesimama pembeni ya Rais ni mdogo wa marehemu Makongoro Nyerere.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya marehemu John Nyerere nyumbani kwao Msasani jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye John Nyerere kilichotokea juzi .Mwili wa Marehemu John Nyerere rubani wa zamani wa ndege za kivita nchini aliyeshiriki kikamilifu vita vya Uganda kati ya mwaka 1978 na 1979, unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda kijijini Butiama mkoani Mara kwa maziko.(picha na Freddy Maro).
Afisa mahusiano Mkuu wa TEITI, Catherine Mbatia akimkaribisha rasmi Mwenyekit wa TEITI, Jaji Mark Boman kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Warsha hiyo iliyowakutanisha wandishi wa habari za biashara na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa madini.
6
Meneja Mahusiano, Alex Modest, (kulia)akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika semina hiyo watatu kulia ni Meneja mikakati kutoka (TBDC) George Kibakaya (kushoto) Mwenyekiti TEITI,Jaji Bomani,wa pili kushoto mwandishi mchambuzi, John Bwire,(katikati) ni Halfani Halfani kutoka (Oil Gas Association Tanzania-OGAT).
2
Afisa mahusiano Mkuu wa TEITI, Catherine Mbatia akielezea juu ya TEITI, wakati wa Warsha hiyo iliyowakutanisha wandishi wa habari za biashara na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa madini.
13
Mwenyekiti TEITI, Jaji Bomani (kushoto ) akichangia mada katika warsha hiyo, wengine ni Mwanahabari na mchambuzi John Bwire, akifuatiwa na Halfani Halfani wa OGAT, Meneja mikakati kutoka (TBDC) George Kibakaya pamoja na Godvictor kutoka kampuni ya madini ya Geita.
14
Wadau wa sekta ya madini na wanahabari wakifuatilia mada katika warsha hiyo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog