Tuesday, May 12, 2015


FIFA
  • Wachezaji watatakiwa kuonesha pasi zao halisi za kusafiria (passport) kabla ya mechi ili kuhakikisha kama wanastahili.
FIFA imerekebisha sheria zake, ikiwa pamoja  na kufuta  maamuzi ya  kurudia mechi nzima ya kufuzu Kombe la Dunia ambayo ilivunjika/iliishia katikati (haikufika dakika 90), kwa sasa mechi iliyovunjika itaanzia katika dakika ya mwisho wakati mechi inavunjika.
Wachezaji watatakiwa kuonesha pasi halisi za kusafiria massa 24 kabla mechi haijaanza kama uthibitisho wa kustahili kulichezea taifa husika.
Mwaka 2014, Uongozi wa FIFA ulithibika kuwa na udhaifu mkubwa hasa  kwa kushindwa kuwatambua wachezaji waliokuwa hawastahili  kuchezea baadhi ya nchi katika mechi za makundi.
Africa lilikuwa ni Bara pekee, kati ya mabara sita wanachama wa FIFA lililokuwa na matatizo katika kuidhinisha uhalali wa wachezaji.
Mataifa saba ya Africa – Burkina Faso, Equatorial Guinea, Ethiopia, Gabon, Liberia, Sudan and Togo –  yalichezesha wachezaji ambao hawakuweza kuthibitisha uhalali wao, kitu kilicholazimisha FIFA kuwazawadia wapinzani wao ushindi wa 3-0.

Hizi ndizo sheria za FIFA zilizobadilika kwa ajili ya Kombe la Dunia 2018:
  • FIFA inataka mechi zote zilizovunjika (zilizoishia katikati, kabla ya dakika 90), zichezwe tena katika tarehe ya mbele na vikosi vilevile na zianzie katika dakika ileile ilipoishia wakati mechi inavunjika. Kabla ilikuwa mechi inarudiwa dakika 90.

  • Mchezaji asiye na pasi halisi ya kusafiria hataweza kucheza mechi. Vitambulisho au nyaraka zozote rasmi za kiserikali hazitakubaliwa.

  • FIFA imefuta kikomo cha faini ya Franc milioni moja za Uswisi (zaidi ya Tsh. bilioni moja na Milioni 900) kwa mashirikisho endapo timu iliyofuzu fainali za Urusi itatolewa siku 30 kabla ya mashindano kuanza au wakati mashindano yanaendelea.

  • Teknolojia ya kugundua goli (Goal-line technology) itaweza kutumika katika mechi za kufuzu endapo timu zitakubaliana kwa maandishi.

  • Vipindi vya kutulia kidogo (Cooling breaks) vitaamuliwa na refa katika mechi za kufuzu.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog