Shuhuda Patrick ambae ni mtangazaji wa Radio aliekua kwenye gari nyuma ya moja ya haya mabasi anasema wenye makosa ni madereva wa mabasi ambao walikua kwenye mwendo kasi na kushindwa kupishana kwenye daraja ambalo ni dogo, daraja lisiloruhusu mabasi mawili kupishana.
Shuhuda mwingine anasema Mabasi haya mawili yalikua yakipigiana honi kutambiana kila mmoja amwache mwenzake apite hivyo mwenye Mwanza Coach alikua anaamini huyu wa J4 angempisha apite darajani vivyohivyo kwa mwenye J4 alikua anaamini huyu wa Mwanza coach angemwachia apite kwa hiyo huo mchanganyiko ndio ukawafanya wagongane katikati ya daraja na kuligonga gari dogo lililotumbukia darajani.
0 maoni:
Post a Comment