Pamoja
na idadi ya matukio mengi ya Majambazi Tanzania imekua ni nadra sana
kusikia Majambazi wamevamia kituo cha Polisi na kusababisha mauaji ya
askari pamoja na kuiba silaha.
Kwa mujibu wa Radio One, hii imetokea kwenye mkoa mpya wa Geita katika kituo cha Polisi Bukombe ambapo Majambazi hawa walivamia na kuwauwa askari polisi wawili na wengine wawili kujeruhiwa na kisha kuiba silaha kadhaa kutoka kwenye kituo hicho.
Majambazi wameingia kwenye rekodi za matukio makubwa 2014 baada ya wengine wanaoaminika kuwa raia wa Burundi, kuirushia daladala bomu la kutupa kwa mkono huko Kigoma baada ya daladala hiyo kugoma kusimama iliposhtukia mchezo wa kutaka kutekwa hivi karibuni.

0 maoni:
Post a Comment