Maisha yamebadilika: Kiungo Cesc Fabregas alijiunga na Chelsea akitokea Barcelona
CESC Fabregas amekiri kuwa bado
anajihisi kama mchezaji wa Arsenal-licha ya kujiunga na wapinzani wao wa
London, klabu ya Chelsea kwa paundi milioni 30 majira ya kiangazi mwaka
huu.
Kiungo huyo mshambuliaji wa Hispania
tayari ameshaonesha makeke Stamford Bridge kwa kutoa pasi za mwisho nne
kwa wachezaji wenzake msimu huu.
Baada ya kuondoka katika klabu yake
aliyokulia ya Barcelona-Fabregas anatarajia kurudi katika klabu yake ya
zamani ya London Kaskazini akiwa na mkanda mpya wa Chelsea.
Enzi zake: Fabregas, ambaye aliichezea Arsenal kwa miaka 8, amesema siku zote anajihisi kama mchezaji wa Gunners
Furaha: Kiungo wa Hispania, Fabregas (kushoto) akishangilia bao la Chelsea dhidi ya Everton mapema msimu huu.
"Kwa wakati wote nitajihisi kama mtu wa
Gunners na najua narudi pale (uwanja wa Emirates) na nahisi utakuwa
wakati maalumu, lakini nimejifunga na Chelsea," Fabregas aliwaambia El
Pais.
"Kumbuka nilicheza fainali ya ligi ya
mabingwa dhidi ya Barcelona! naapa kwamba nilifanya kila kitu
kuhakikisha tunashinda mechi ile hata kama nilikuwa Barcelona tangu
utotoni"
0 maoni:
Post a Comment