Nje: Reus akiugulia maamuzi katika mechi ya jana usiku dhidi ya Scotland
NYOTA wa Borussia Dortmund, Marco Reus
ataikosa mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Arsenal huko
Westfalenstadion kufuatia kuvunjika mfupa wa kifundo cha mguu katika
mechi ya kuwania kufuzu fainali za Euro 2016 dhidi ya Scotland.
Mkali huyo wa Ujerumani atakaa nje ya uwanja kwa wiki nne baada ya kukatwa buti na Charlie Mulgrew jana usiku.
Arsenal watasafiri kwenda Ujerumani
Septemba 16 mwaka huu kukabiliana na Dortmund katika mechi ya makundi ya
ligi ya mabingwa-kwa mara ya nne ndani ya miaka minne ambapo klabu hizo
zinapangwa kundi moja na Reus atarudi uwanjani mpaka mapema mwezi
oktoba.
Balaa gani?: Winga wa Ujerumani akianguka chini baada ya kukatwa buti na Charlie Mulgrew na kuumia kifundo cha mguu wa kushoto
Atakosekana: Klabu ya Reus ya Borussia Dortmund ilitangaza taarifa hizo katika mtandao wa Twita.
0 maoni:
Post a Comment