Daniel Sturridge atakaa nje ya uwanja kwa wiki tatu baada ya kupata majeruhi katika mazoezi ya England
BRENDAN Rodgers ameponda matibabu wanayotoa England kwa mshambuliaji wake Daniel Sturridge baada ya kupata majeruhi ya mguu.
Sturridge aliumia ijumaa iliyopita, saa
48 baada ya kucheza dakika 89 katika ushindi wa England wa bao 1-0 dhidi
ya Norway katika mechi ya kimataifa ya kirafiki.
Nyota huyu alikosa mechi ya kuwania
kufuzu Euro 2016 dhidi ya Uswizi ambapo England ilishinda mabao 2-0 na
sasa yuko nje ya uwanja kwa wiki tatu.
Rodgers amechukia sana kwasababu mshambuliaji wake hakupewa muda mzuri wa kupumzika.
"Tumekatishwa tamaa sana kwasababu tunadhani majeruhi yake ingetibiwa haraka," Bosi wa Anfield alisema.
+5
Daniel Sturridge amemtia hasara kocha wake Brendan Rodgers
Daniel Sturridge akionesha ufundi wake katika mazoezi ya England dhidi ya Phil Jones kabla ya kuumia
0 maoni:
Post a Comment