Monday, August 11, 2014



Kocha wa Man City Manuel Pellegrini asisitiza timu yake itatetea taji lake
Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema anamatumaini makubwa timu hiyo italitetea taji lake licha ya kuambulia kichapo cha mabao matatu kwa nunge dhidi ya vibonde wao Arsenal katika mechi ya kuwania ngao ya Community hapo jana. Good day out: Mikel Arteta lifts the Community Shield after a thumping win over the Premier League champions
Man City, wameratibiwa kufungua kampeini ya kutetea taji lao dhidi ya Newcastle jumapili ijayo.
Baada ya kichapo hicho hiyo jana Pellegrini aliulizwa na BBC Michezo iwapo anamatumaini kuwa timu hiyo inauwezo wa kutetea taji lake Pellegrini alisema kwa kinywa kipana ndiyo.

'' Nafahamu kuwa msimu huu timu 5 au hata 6 zinauwezo wa kutwaa taji la ligi msimu huu lakini nakuhakikishia kuwa kati ya timu hizo zote Man city ndiyo inatimu yenye uwezo wa kushinda.'' alisema Pellegrini.
''Wajua ni vigumu kuamini lakini mkitupa muda tutawathibitishia hilo uwanjani''.
Man City iliambulia kichapo cha 3-0 dhidi ya Arsenal.


Pellegrini alisema kutokuwepo kwa mshambulizi wake machachari Sergio Aguero mlinzi Vincent Kompany, Pablo Zabaleta na Bacary Sagna liathiri mchezo wetu.
''Unafahamu kuwa kikosi kilichocheza hivi leo sio kikosi chetu cha kwanza ''.

Pellegrini alimpa nafasi ya kuanza mchezaji mpya Willy Caballeroin na akamwelezea kipa nambari moja msimu uliopita Joe Hart, kuwa lazima adhihirishe uwezo wake msimu huu kwani anaupinzani si haba.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog