LICHA
ya kuwa miongoni mwa wachezaji wachache wa England waliorudi na heshima
kutoka kombe la dunia, Raheem Sterling amesisitiza kuwa anahitaji
kuonesha kiwango kikubwa katika klabu yake ya Liverpool msimu ujao.
Nyota
huyo kinda mwenye miaka 19 alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Liverpool
waliokaribia kutwaa ubingwa wa ligi kuu ambapo walimaliza pointi mbili
nyuma ya mabingwa Manchester City.
Kivutio: Raheem Sterling amekuwa na mvuto tangu alipowasili katika kambi ya Liverpool iliyopo Boston.
Sterling
amejiunga na kambi ya mazoezi iliyopo Boston akijua wazi kuwa
kusajiliwa kwa wachezaji wapya kunamaanisha nafasi yake haina uhakika.
Akizungumza
na LFCTour.com, alisema: “Bado natakiwa kujithitisha mwenyewe, kocha
ameleta wachezaji ambao wenye uwezo wa kucheza nafasi kama yangu,
natakiwa kumuonesha kocha na kujituma zaidi ili kupata namba ya kudumu
katika timu”.
0 maoni:
Post a Comment