Friday, July 25, 2014




Mabaki ya ndege iliyopotea ikiwa na watu 116 njiani kutoka Burkanafaso kwenda Algers yamepatikana nchini Mali.
Maafisa wa Jeshi wa Burkina faso wamesema ndege hiyo iliyokuwa chini ya shirika la ndege la Algeria imeanguka karibia kilomita 50 kutoka mpaka wa Burkanafaso.
Waongoza ndege walipoteza mawasilino na ndege hiyo muda mfupi baada ya kupata taarifa kutoka kwa Rubani kuwa alikuwa kwenye eneo lenye hali mbaya ya hewa.
Utafutaji wa ndege hiyo umeanzia katika eneo la Gao mpaka Tessalit. Kumekuwepo na hali mbaya ya hewa kwa zaidi ya saa 24. Waziri wa mambo ya nje wa ufaransa, Laurent Fabius amesema inaonekana ndege ilihamishwa mwelekeo kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.
„Walikuwa wameelekezwa kubadili njia ya kawaida kutoka na mabadiliko ya hali ya hewa.Ndege ilikuwa ikipaa juu ya eneo la Malian. Pamoja na juhudi kubwa , mapaka sasa hakuna dalili za kupatika na kwa ndege hiyo. Pengine ndege imeangua"

Ameongeza kuwa waziri wa ulinzi wa ufaransa alikuwa akisaidia katika utafutaji wa ndege hiyo.
"Waziri wa ulinzi wameviruhusu vyombo vyao kwenda kwenye eneo kuitafuta ndege. Majeshi ya Algeria na Umoja wa mataifa wanafanya hivyo pia. Ndege mbili za jeshi la ufaransa zilizopiga kambi Niyame hivi sasa na tangu asubuhi zimekua zikiitafuta ndege hiyo. Majeshi yetu katika eneo hilo ikiwamo vifaa vya matibabu vyote viko tayari"

Hapo awali, waziri mkuu wa Algeria Abdelmalek Sellal alitoa ufafanuzi wa tukio la kuanguka kwa ndege hiyo.
"Usiku wa jana kama saa 9 ndege ya Hispania iliyokodiwa na Shirika la Ndege la Algeria ilikuwa katika safari yake kati ya Ouagadougou na Algiers. Ilipoteza mawasiliano na Rada muda huo wa saa tisa usiku dakika 10 tu baada ya kupaa. Mawasiliano ya mwisho ilikuwa na mnara wa kuongozea ndege ulioko Niger na ndege ilikuwa juu ya Gao, kama kilomita 500 kutoka kwenye mpaka wa Algeria. Kulikuwa na abiria 119 wakiwamo wafanyakazi wake. Utafutaji bado unaendelea na tunawasiliana na mamlaka zinazohusika. Waliokuwa kwenye ndege ni raia wa Algeria pamoja na mataifa mengine"

Mamlaka zinazohusika nchini Burkina Faso ambako ndiko ndege ilitokea wameamua kutoa msaada wa kisaikolojia kwa wanafamilia wa wale waliokuwa katika ndege. Baadhi ya ndugu wamefika katika uwanja wa ndege wa Ouagadougou kufuatilia taarifa kuhusu ndugu zao. Baadhi walikuwa na malalamiko
"Tuwanataka watuambie kama ndege hiyo imeanguka, kuna walionusurika, au wote wamekufa. Hayo ndio tunayotaka kujua. Tupo kwenye wakati mgumu. Watatu miongoni mwetu, tulitaka kusafiri na dada yetu lakini tuliamua kuahirisha safari katika dakika za mwisho. Hata hivyo dada yetu yeye aliondoka usiku jana."
Mwaume mwingine aliyekuwepo kwenye uwanjahuo wa ndege alisema

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog