Wednesday, June 11, 2014


Roy Hodgson ana matumaini makubwa Alex Oxlade-Chamberlain atakuwa fiti kucheza Mechi ya England ya Pili ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay.
Winga huyo wa Arsenal hataweza kucheza Mechi ya Kwanza na Italy hapo Jumamosi Juni 14 huko Manaus, Brazil baada ya kuumia Goti walipocheza na Ecuador huko Miami, Florida Nchini Marekani Wiki iliyopita.
Akithibitisha kwa Mchezaji huyo mwenye Miaka 20 kuweza kuikabili Uruguay huko Sao Paulo, Hodgson alisema: “Anaendelea vizuri sana na Mazoezi yake binafsi Wiki yote hii!”
Wakati huo huo kuliibuka Ripoti kuwa Nahodha wa England Steven Gerrard ana maumivu ya Nyonga lakini Kocha wa England, Hodgson, amezipiga chini stori hizo.

Amesema: “Tulifanya Mazoezi Jana na kutenganisha wale Wachezaji waliocheza Jumamosi na wale ambao hawakucheza ili kuwapa Programu tofauti. Mwishoni, Steven alifanya Mazoezi ya ziada. Hana tatizo na sielewi Stori hizo!”



ENGLAND KWENYE KUNDI
KUNDI D

14 Juni: England v Italy, Manaus
19 Juni: England v Uruguay, Sao Paulo
24 Juni: England v Costa Rica, Belo Horizonte

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog