Wednesday, June 11, 2014


Refa NISHIMURA Yuichi na wasaidizi wake SAGARA Toru na NAGI Toshiyuki
REFA kutoka Japan Yuichi Nishimura amepangwa kuchezesha Mechi ya Ufunguzi ya Fainali zaKombe la Dunia kati ya Wenyeji Brazil na Croatio itakayochezwa Alhamisi Juni 12 huko Arena Corinthians, Jijini Sao Paulo.

Wasaidizi wake ni kutoka Japan ambao ni Toru Sagara na Toshiyuki Nagi huku Alireza Faghani wa Iran akiwa ni Refa wa Nne.
Sambamba na hao, FIFA pia imetangaza Marefa wa Mechi 3 nyingine za mwanzoni.
Nishimura, mwenye Miaka 42, anakuwa Refa wa Tatu kutoka Japan kuchezesha Fainali za Kombe la Dunia mara mbili wengine wakiwa Shizuo Takada (1986 na1990) na Toru Kamikawa (2002 na 2006).
Kwenye Fainali za 2010 huko Afrika Kusini, Nishimura alichezesha Mechi 4 ikiwemo Robo Fainali kati ya Netherlands na Brazil.
Mwaka 2012, Yuichi Nishimura alitajwa kuwa ndie Refa Bora wa Mwaka wa AFC, Shirikisho la Soka la Asia.



KOMBE LA DUNIA
RATIBA-Mechi za Ufunguzi:

Alhamisi 12 Juni 2014
KUNDI A

23:00 Brazil v Croatia
-REFA: Yuichi Nishimura [Japan]

Ijumaa 13 Juni 2014
19:00 Mexico v Cameroon
-REFA: Wilmar Roldan [Colombia]

KUNDI B
22:00 Spain v Netherlands
-REFA: Nicola Rizzoli [Italy]
01:00 Chile v Australia
-REFA: Noumandiez Doue [Ivory Coast]

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog